• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

Video

  • KAMPENI YA UPIMAJI HALI YA LISHE KWA WATOTO YAZINDULIWA.

    June 12th, 2024

    Mkoa wa Iringa ambao ni kinara kwa uzalishaji wa vyakula sasa inaondokana na hali ya udumavu ambapo Mkuu wa Mkoa , Mhe. Peter Serukamba amezindua kampeni maalum ya kupima hali ya lishe kwa Watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 ambapo kwa Mkoa mzima ni watoto 2,059,204/= ili kubaini viashiria vya udumavu


    Kampeni hiyo imezinduliwa na kuanza rasmi leo Juni 12,2024 katika vituo vyote vya afya vilivyo ainishwa .


    Akizungumza katika kikao cha kamati ya afya ya msingi Mhe. Serukamba amesema kuwa kuhusu kampeni maalam ya kutathimini hali ya lishe kwa Watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 itakayofanyika kuanzia leo mpaka Juni 15,2025 kwa Mkoa mzima.


    “Kinachotakiwa kwenu Wajumbe ni kutoa hamasa katika jamii, kusimamia shughuli za kampeni,kushirikiana na Wadau mbalimbali ili kufikia maendeleo na kufanikisha zoezi la ufanyaji wa tathmini ya hali ya lishe kwa Watoto Mkoani Iringa na kuepusha upotoshaji wowote utakaoweza kujitokeza lakini pia Wajumbe wa kamati hii mnapswa kuhakikisha mnakanusha taarifa za upotoshaji unaoweza kujitokeza katika kampeni hii ”


    Kwa upande wake Afisa lishe wa Mkoa wa Iringa ,Anna Nombo amesema timu ya Wataalam 343 kwa Mkoa watafanya vipimo ili kutathimini hali ya lishe na kupima kimo au urefu, uzito pamoja na mzingo wa kati wa sehemu ya juu ya mkono,kuangalia hali ya chanjo, kuangalia uwepo wa uvimbe mbonyeo katika miguu yote miwili , uwepo wa magonjwa sugu,ulemavu , hali ya ukamilishaji wa umezaji wa dawa za minyoo na kutambua uelewa wa malezi ya watoto.


    Pia ameongeza kwa kusema kuwa baada ya mtoto kupimwa , mtoa huduma atatakiwa kufanya tafsiri ya hali ya lishe ya mtoto husika ndipo mtoto atakayekutwa na hali duni ya lishe mzazi wake atatakiwa kufatiliwa namna ya malezi yake na ulishaji wa mtoto wake kupitia dodoso maalum ili itakapofikia hatua ya utatuzi kuweza kuitatua changamoto hiyo.

  • WAFANYABIASHARA WA SOKO LA MAFINGA WAFIKIA MAKUBALIANO NA MKUU WA MKOA KWA KWA KUSAINI MKATABA

    May 22nd, 2024

    Baada ya Agizo alilolitoa hapo jana Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba akiwa kwenye baraza la Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Mafinga la kumtaka Mkurugenzi kusimamia ubomoaji wa vibanda 331 katika soko la mafinga kutoka na kitendo cha wafanyabiashara wa soko hilo kushindwa kutekeleza agizo la kusaini mkataba ndani ndani ya siku 20, Kufuatia agizo hilo uongozi wa wafanyabiashara ulilazimika kukutana na Mkuu wa Mkoa na kufanya nae mazungumzo na kumwomba kusitisha uamuzo huo wa kubomoa vibanda na badala yake azungumze na wafanyabiashara wote ili kufikia makubaliano ya pamoja jambo ambalo limetekelezwa huku Mkuu wa Mkoa akiwataka wafanyabiashara kusaini mkataba hadi kufikia jumatatu ya mei 27,2024 huku wakitakiwa kuanza kulipa kiasi cha shilingi Elfu 80 kwa mwezi kwa kila kibanda makubaliano ambayo utekelezaji wake utaanza juni mosi mwaka huu.Awali wafanyabiashara hao walikuwa wakilipa kati ya shilingi elfu tatu mpaka elfu tisa kwa mwezi jambo lililoikosesha mapato Halmashauri ya mji wa Mafinga na kuibua mgogoro uliodumu kwa muda wa miaka 15 huku Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba akitumia siku 21 kumaliza mgogoro huo   jambo lililowafurahisha wafanyabiashara hao.

  • RC SERUKAMBA AAGIZA KUVUNJWA VIBANDA 331, SOKO LA MAFINGA

    May 20th, 2024

    Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ametoa masaa 24 Kwa wafanyabiashara wanaomiliki vibanda katika soko la Mafinga kuvunja vibanda 331 vilivyojengwa kimakosa katika eneo linalomilikiwa na Halmashauri ya Mji Mafinga ambavyo husababisha hasara ya zaidi ya Millioni Kumi Kwenye Halmashauri hiyo.Hayo yamejiri  wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika soko hilo akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na MkoaMhe. Serukamba amesema kuwa Halmashauri haiwezi kuendelea endapo hakuna mapato yoyote yale yanayoingia katika Halmashauri hivyo amesema kuwa  hawajalipa kodi kwa zaidi ya miezi sita basi wapishe kwenye eneo hilo la Halmashauri Hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwanza kuzungushia utepe kwenye eneo hilo ili vibanda hivyo viweze kubomolewa."Kwahiyo nimetoa maelekezo watakuja kufunga liboni tanesco wataondoa umeme ili kesho kutwa tunaanza kubomoa vibanda vyote ili tubakie na ardhi yetu halafu baada ya hapo tutajua tunalipangaje soko letu na tutaanza kufanya biashara na wale ambao watahitaji kufanya biashara na sisi"Nae Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dkt. Linda Salekwa amesema kutokana na kukosa Mkataba wafanyabiashara hao wamekosa leseni na kupelekea Halmashauri hiyo kukosa mapatoKwa upande mwingine Mkuu wa Idara ya Viwanda na Biashara wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndg. Evance Mtikile suala la mgogoro wa mkataba kati ya wafanyabiashara hao na Halmashauri limeanza tangu mwaka jana  ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakigomea mkataba huo na kupelekea Halmashauri hiyo kukosa mapato.

  • ← Prev
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • Next →

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DKT. BITEKO AMWAKILISHA RAIS SAMIA UWEKWAJI WAKFU ASKOFU MTEULE JIMBO LA IRINGA

    April 27, 2025
  • KARIBU MKOA WA IRINGA NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI MHE. DOTO BITEKO

    April 26, 2025
  • MIRADI YA MAENDELEO YENYE DHAMANI YA ZAIDI YA BILLIONI 30 KUPITIWA NA MWENGE WA UHURU MKOA WA IRINGA

    April 24, 2025
  • RC SERUKAMBA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUMUAGA BI. ANNA KIBAO ALIYEKUWA MTUMISHI WA OFISI YA MKUU WA MKOA IRINGA

    April 19, 2025
  • Tazama zote

Video

WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

Tovuti Linganifu

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.