• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

WANUFAIKA WA TASAF IRINGA MANISPAA WATAKIWA KUJITATHMINI

Posted on: August 30th, 2017

Wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini kupitia TASAF Manispaa ya Iringa wametakiwa kutathmini manufaa waliyopata kupitia fedha wanazopewa na mpango huo.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipofanya ziara maalum ya kuwatembelea wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini katika mtaa wa Ngelewala uliopo Kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa leo.

Masenza alisema “kila mnufaika anayepokea pesa za TASAF lazima ajitathmini, fedha hizo zimemsaidia nini? Kama hakuna basi ujue ipo kasoro”. Alisema kuwa serikali inatoa pesa hizo ili ziwasaidie wanufaika kuondoka katika hali duni ya maisha kuelekea hali bora. Alishauri kuwa pesa hizo zitumike kwa uangalifu ili zilete matokeo yaliyokusudiwa.

Mkuu wa mkoa aliwataka watendaji wa mitaa kuwa karibu na wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini ili kuwasaidia na kuwashauri vizuri. “Ni jukumu la kila mtendaji wa mtaa kujua hitaji la kila mnufaika wa TASAF. Wapo wanufaika wanaotaka kufuga lakini hawajui wanaanzia wapi, wapo wanufaika wanaohitaji kulima lakini hawajui waanzie wapi, hivyo kuwa nao karibu kutawasaidia kufikia malengo yao” alisema Masenza.

Akiwasilisha taarifa fupi ya mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF awamu ya tatu, mratibu wa TASAF Manispaa ya Iringa, Lucy Mtafi alisema kuwa mpango huo umelenga kuziwezesha kaya masikini kupata mahitaji ya msingi na fursa za kuongeza kipato, kulinda rasilimali zao na kuweka akiba kwa ajili ya kujiletea maendeleo na hatimae kujitoa katika umasikini.

Mtafi alisema kuwa mitaa ya Mawelewele na Ngelewala inayotembelewa na mkuu wa mkoa ina wanufaika 77 ambao walipokea ruzuku ya shilingi 28,928,000.

Akiongelea mafanikio yaliyopatikana, mratibu wa TASAF Manispaa ya Iringa, aliyataja kuwa ni kuongezeka kwa mahudhurio ya wanafunzi shuleni kutoka 80% hadi 99%. Aliongeza kuwa wazazi wamemudu kununua mahitaji ya watoto ya shule. Mafanikio mengine aliyataja kuwa ni mahudhurio ya kupima watoto kliniki yameongezeka kwa 90% na elimu ya lishe bora imetolewa kwa akina mama wanapohudhuria kliniki. Jumla ya kaya 2,302 zimejiunga na mfuko wa tiba kwa kadi (TIKA) na wanufaika wa wamemudu kupata mahitaji ya msingi kama milo mitatu kwa siku. Mengine ni wanufaika kuanzisha biashara ndogondogo na ufugaji wa kuku na nguruwe.  

Mpango wa kunusuru kaya masikini katika Manispaa ya Iringa ulizinduliwa tarehe 6/1/2015.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA - 2023 December 17, 2022
  • MAADHIMISHO YA KARIBU KUSINI MWAKA 2022 September 19, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KONGAMANO LA FUNDI SMART LAFANYIKA LEO IRINGA .

    March 17, 2023
  • Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima O. Dendego akifungua kikao cha kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika leo tarehe 25/03/2023 katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya İringa

    March 14, 2023
  • TUNATAKA KUONA MAPINDUZI YA KIJANI KATIKA MKOA WA IRINGA: RC DENDEGO

    February 28, 2023
  • FANYENI KAZI KUWAHUDUMIA WANANCHI

    February 21, 2023
  • Tazama zote

Video

UZINDUZI WA ZAHANATI YA ITAGUTWA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Pawaga Road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, Iringa

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2021, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.