• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

Wafanyakazi Rasilimali Muhimu Uchumi wa Viwanda- Waziri Mwijage

Posted on: April 28th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Wafanyakazi ni rasilimali muhimu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kukuza pato la nchi ikilinganishwa na rasirimali nyingine zote.

Kauli hiyo ilitolewa na waziri wa viwanda na biashara, Charles Mwijage alipokuwa akifungua kongamano la Tanzania ya viwanda lililofanyika katika ukumbi wa Kichangani mjini Iringa jana.

Waziri Mwijage alisema kuwa nchi ina rasilimali nyingi sana. Rasilimali muhimu aliitaja kuwa ni rasilimali wafanyakazi. Alisema kuwa wafanyakazi ni muhimu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kukuza pato la taifa.

Akiongelea uchumi wa kati, waziri huyo alisema kuwa uchumi wa kati unategemea shughuli za watu katika kujenga viwanda vinavyochakata na kusindika malighafi za mazao ya shamba. Dhamira ya serikali ni kuhakikisha nchi inakuwa na sekta ya viwanda iliyo imara, shindani na endelevu. Alisema kuwa viwanda vinavyoongelewa siyo viwanda vya kufa kama binadamu, bali ikitokea vikafa, vinazaliwa vingine na kuendeleza nyororo wa thamani. Alisema kuwa watu wengi wamekuwa na mtazamo tofauti wa dhana ya kiwanda, alisisitiza kuwa mtu akiwa na cherehani nne hicho tayari ni kiwanda kidogo. Viwanda vidogo vinasaidia kupunguza kusafirisha mazao na hatari ya mazao hayo kuharibika wakati wa usafirishaji wake.

Waziri Mwijage alitoa wito kwa jamii kuwashawishi wafanyakazi kuanzisha viwanda tofauti na utaratibu wa sasa wa kukopa kwa ajili ya kununua magari. Aidha, alizitaka mamlaka za serikali za mitaa kutenga maeneo kwa ajili ya uanzishwaji wa viwanda. Alishauri viwanda vinavyoanzishwa viwe vinavyoongeza thamani.

Waziri Mwijage, alisema kuwa mipango iliyopo ni kuufanya uchumi ujikite katika maendeleo ya watu. “Uchumi tulionao ni wa maendeleo ya vitu zaidi kuliko maendeleo ya watu, hivyo tunataka kufanya mageuzi ya maendeleo ya watu ambayo yanapimwa kwa vitu vitatu”. Alivitaja vitu hivyo kuwa ni elimu, afya na kipato kitakachopatikana kutokana na uchumi wa viwanda.

Alisema kuwa serikali inajukumu la kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji.

=30=


Matangazo

  • MAADHIMISHO YA UTALII KARIBU KUSINI 2023 May 01, 2023
  • MAADHIMISHO YA KARIBU KUSINI MWAKA 2022 September 19, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI DANIEL CHONGOLO AMEMUAGIZA MKUU WA MKOA WA IRINGA HALIMA DENDEGO KUHAKIKISHA MPAKA KUFIKIA JULAI MOSI MWAKA HUU KITUO CHA AFYA CHA BANDA BICHI KIWE KIMEFUNGULIWA

    June 01, 2023
  • KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), DANIEL CHONGOLO AMEITAKA SERIKALI KUHARAKISHA MCHAKATO WA MABADILIKO YA MITAALA YA ELIMU

    May 28, 2023
  • TANZIA

    May 21, 2023
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI

    May 11, 2023
  • Tazama zote

Video

UZINDUZI WA ZAHANATI YA ITAGUTWA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2023, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.