• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

Viongozi Iringa kupunguza Maambukizi ya Kifua Kikuu-RC Masenza

Posted on: March 25th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Viongozi mkoani Iringa wametakiwa kujipanga kuhakikisha maambukizi ya kifua kikuu yanapungua ili wananchi waweze kutekeleza shughuli za maendeleo.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yaliyofanyika ngazi ya mkoa katika mji wa Ilula wilayani Kilolo jana.

Masenza alisema kuwa viongozi katika ngazi zao wanajukumu la kuhakikisha maambukizi ya kifua kikuu yanapungua katika jamii inayowazunguka ili jamii hiyo iweze kufanya kazi za kuzalisha mali. “Kwa hiyo katika vikao vyote vitakavyofanyika katika maeneo yetu ya kazi, katika ngazi zote kifua kikuu iwe ni agenda ili kuweza kupanga mikakati ya uboreshaji wa huduma za kifua kikuu” alisema Masenza. Aidha, alizitaka Halmashauri katika mkoa wa Iringa kupanga na kufanya shughuli za uchunguzi wa dalili za kifua kikuu katika makundi hatarishi. Aliyataja makundi hayo kuwa ni shule, magareza na maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu.

Mkuu wa mkoa alisema kuwa katika kuadhimisha juma la siku ya kifua kikuu duniani, katika eneo la Ilula Sokini, huduma mbalimbali zilikuwa zikitolewa kwa wananchi bila malipo. Huduma hizo alizitaja kuwa ni uchunguzi wa dalili za kifua kikuu na matibabu, upimaji wa maambukizi ya VVU, uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi, uchangiaji na utoaji wa damu, huduma ya uzazi wa mpango, elimu kuhusu lishe, na elimu kuhusu kifua kikuu.

Maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yamefanyika ngazi ya mkoa katika mji wa Ilula yakiongozwa na kaulimbiu isemayo ‘viongozi tuwe mstari wa mbele kuongoza mapambano ya kutokomeza kifua kikuu’.

=30=



Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC SERUKAMBA AMESHIRIKI NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA MDOGO WAKE NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU MHE WILLIAM LUKUVI

    June 07, 2025
  • WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA

    June 06, 2025
  • MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA KITAIFA YATAFANYIKA MKOA WA IRINGA

    June 02, 2025
  • KAMBI YA MADAKTARI BINGWA YA MAMA SAMIA YATUA IRINGA

    June 02, 2025
  • Tazama zote

Video

WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.