Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter amemuagiza mhandisi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kuweka kambi katika ujenzi wa kituo cha afya cha Mlenge ili kufikia Tarehe 30/05/2024 ujenzi wa majengo hayo mawili uwe umekamilika
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua Miradi katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa ambapo amewapongeza wananchi kwa kujitoa kwao katika ujenzi wa kituo hicho na kutoa maagizo kwa mhandisi wa Halmashauri kuanzia sasa asikae ofisini na badala yake aweke kambi katika ujenzi wa kituo hicho
Nao baadhi ya wananchi wameishukuru Serikali kwa ujenzi wa majengo mawili ya kituo hicho cha afya ambacho kimegharimu Shilingi Millioni Mia Tatu thelathini na Tisa na kusema kuwa kwasasa wameondokana na adha ya kwenda umbali mrefu kwajili ya kupata huduma za kiafya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.