Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ametoa ushauri kwa kwa Halmashauri ya Mji Mafinga kuongeza Majengo katika Kituo cha Afya cha Upendo.
Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua miradi iliyopo katika Halmashauri hiyo.
Akizungumza katika mradi huo wa kituo cha afya cha Upendo kilichopo katika Kata ya Upendo Mhe. Serukamba amesema kuwa kwa majengo yakiyopo hapo bado hayajitoshelezi hivyo amewataka kuongeza majengo mawili kwa fedha za ndani ili kituo hicho kipate hadhi ya kuitwa kituo cha Afya
Pia ameushauri Halmashauri hiyo kuachana na ujenzi wa miradi midogo midogo kwenye kata na badala yake kwa kila mwaka wawe na mpango wa kujenga mradi mmoja mkubwa wa kimkakati ambao utakuwa wenye manufaa makubwa kwa wananchi.
Sambamba na hayo Mhe. Serukamba ameipongeza Halmashauri hiyo kwa miradi mizuri waliyonayo ambayo na kwa baadhi ya miradi amewataka mafundi kuimaliza kabla ya mwezi ujao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.