Mhe Halima Omary Dendego, Mkuu wa Mkoa Iringa Leo ameongoza mdahalo wa madhimisho ya 16 ya kupinga ukatilii wa kijinsia katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Mhe Rc Dendego, amewataka wanazuoni hao kuishi kwa misingi ya imani zao maana Leo kumekuwa na matukio mengi ya ukatilii, ubakaji na ulawiti ambao umekithiri kwa wingi hususani mkoani iringa.
"Leo ukipita vyuoni uko au mitaani utaona mabinti wamevaa nusu uchi je kweli mtashindwa kubakwa? Huo sio ujanja ni ushamba jitunzeni vijana mpaka muda wako ukifika wa kuoa au kuolewa"
Naye Mstahiki Meya Mhe Ibrahim Ngwada, kabla ajamkaribisha Mkuu wa Mkoa amesema kuwa tumeamua kuandaa mdahalo huu wa kupinga ukatilii wa kijinsia kwa wanazuoni kwa sababu kumekuwa na matukio mengi ya ukatilii hapa Manispaa ya iringa kwa sababu ukatilii huu kwa namna nyingine unasababishwa na waganga wa kienyeji kwa kuwadanganya wateja wao kuwa wakizini na watoto bikra wanapata utajiri, kumbe ni uongo.
Nae mtaalumu wa saikolojia ndugu Leornad Mgina amewataka wanazuoni hao kuzingatia masoma yao( umakini) maana wengi wanatoka kwenye lengo na kukimbilia starehe. Watu wengi wana tatizo la Afya ya akili ndio inayopelekea kufanya ukatilii wa kijinsia.
Pia mdahalo huo umehudhuriwa na viongozi wa dini, mila na waheshimiwa madiwani wa Manispaa ya iringa.
Imetolewa na Afisa habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.