Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Kamati ya kitaifa ya ushauri wa misitu imetakiwa kuangalia upya takwimu zinazoonesha mchanago mdogo wa sekta ya misiku katika pato la taifa na kumshauri waziri mwenye dhamana juu ya mchango wa sekta ya misitu kuongeza mchango wake.
Kauli hiyo ilitolewa na waziri wa maliasili na utalii, Dr. Hamis Kigwangala alipokuwa akifungua kikao cha tatu cha kamati ya kitaifa ya ushauri wa misitu kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha VETA mjini Iringa jana.
Dr. Kigwangala alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa sekta ya misitu inachangia takribani asilimia 3.7 katika pato la taifa. “Sisi kama wizara haturiziki kabisa na mchango huu. Bado tunaona uko chini sana kiasi cha kutishia kutoaminika kwa takwimu hizo kabisa. Hili tunaona ni eneo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi haraka” alisema Dr. Kigwangala. Aidha, aliitaka kamati hiyo kuja na ushauri wa jinsi ya kuitumia sekta ya misitu katika kuongeza mchango wake katika pato la taifa.
Katika salamu za mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa utalii unakuwa endelevu, Mkoa wa Iringa umefanya utalii kuwa agenda ya kudumu katika vikao vyake. Alisema kuwa Mkoa umejipanga kuendeleza eneo la Kihesa kilolo kwa kukuza utalii kwa kulitunza, kuliendeleza na kulihifadhi. Utunzaji wa eneo hilo utachangia uendelevu wa sekta ya utalii na uhifadhi mkoani Iringa na ukanda wa nyanda za juu kusini, alisema mkuu wa Mkoa.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.