• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe,Halima Dendego atoa maagizo Ewura kushughulikia maslai ya wafanyakazi

Posted on: November 9th, 2022


Mkuu wa wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego ameielekeza Menejimenti ya EWURA kushugulikia maslahi ya Wafanyakazi kwa wakati ili kuondoa malalamiko yanayoweza  kujitokeza sehemu za kazi kwa lengo la kuimarisha utendaji na ufanisi wa utendaji.


Mkuu wa Mkoa mhe Halima Dendego ameelekeza hayo wakati akifungua kikao cha nne cha baraza la Wafanyakazi wa EWURA , leo 9 Novemba 2022 mjini Iringa.


“Menejimenti ya EWURA kuweni karibuni na wafanyakazi wenu, shughulikieni maslahi yao kwa wakati ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima


Mkuu wa Mkoa  amewataka wafanyakazi wa EWURA kuwa na staha wanapo dai maslahi yao na kuwajibika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.


Aidha Mkuu wa Mkoa Mhe Halima Dendego akiwa na RAS Eng, Leonard Masanja wamekabidhi na kupokea hundi zenye thamani ya sh. milioni 10 kwa shule ya Sekondari ya Wasichana Iringa kusaidia ujenzi wa uzio na shilingi milioni 10 nyingine kuunga mkono juhudi za kuimarisha utalii kwa Nyanda za Juu Kusini katika kushamirisha tamaha la “Utalii Karibu Kusisni 2022”


Akizungumzia msaada huo, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mha. Modeatus Lumato, alieleza kuwa, EWURA imekuwa na utaratibu wa kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali na kwamba kipindi hiki Mamlaka imetoa kipaumele katika eneo la elimu na utalii.


“Sisi EWURA, tumeona ni vyema tusaidie kuimarisha miundombinu ya elimu pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan katika masuala hayo.


Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Iringa, Mwl Mikodadi Rashid, baada ya kupokea hundi hiyo,  aliishukuru EWURA kwa msaada huo na kueleza kuwa utakuwa  chachu ya kuboresha mazingira ya kusomea.


Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa Mha.Amani Msuya aliyetoa salamu za TUGHE Taifa kwa niaba ya Katibu Mkuu wake, Henry Mgunda, ameeleza kuwa taasisi zote za umma zinatakiwa kuhakikisha zinakuwa na utaratibu wa kuimarisha maslahi na hali bora za wafanyakazi.


Kwa upande wake Katibu wa TUGHE Tawi la EWURA, Bw. Emmanuel Ndalawa alieleza kuwa, wataendelea kutoa ushirikano kwa menejimenti ya EWURA ili kwa pamoja kuleta tija zaidi

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC SERUKAMBA AMESHIRIKI NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA MDOGO WAKE NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU MHE WILLIAM LUKUVI

    June 07, 2025
  • WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA

    June 06, 2025
  • MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA KITAIFA YATAFANYIKA MKOA WA IRINGA

    June 02, 2025
  • KAMBI YA MADAKTARI BINGWA YA MAMA SAMIA YATUA IRINGA

    June 02, 2025
  • Tazama zote

Video

WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.