Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Queen Sendiga kushirikiana na kamati ya siasa ya mkoa amefanya ziara ya siku mbili katika halmashauri ya wilaya ya mufindi tareh 14-15 Januari 2022 kwa ajili ya kutembelea miradi iliyotekelezwa katika wilaya ya mufindi ambayo ni miradi ya elimu, maji na barabara miradi hii imetekelezwa kwa pesa za UVIKO-19, Tozo na fedha za ndani kutoka kwa wanachi kwa lengo la kuleta maendeleo katika wilaya hiyo.
Miradi ilikabidhiwa kwa mkuu wa mkoa tarehe 11-01-2022 ikiwa imekamilika kwa asilimia mia na ye mkuu wa mkoa amekabidhi miradi hiyo kwa kamati ya siasa mkoa wa Iringa ikiwa ni madarasa miradi ya maji katika vijiji tofauti pamoja na barabara.
Mwenyekiti wa kamati ya siasa mkoa wa Iringa Dr. Abel Nyamahanga amepokea miradi hiyo na kuridhishswa na utendaji kazi wa serikali mkoa wa Iringa.Amepongeza mkuu wa mkoa na team yake yote kwa utendaji na kazi nzuri iliyofanyika katika wilaya ya mufindi
“kwa kipeke tuseme tu kwamba tumeridhika sana na miradi yote ni jambo la kupongeza sana kama chama hatuna malalamiko mkuu wa mkoa nakushukuru sana “ amesema Dr. Nyamahanga
Pia Dr. Nyamahanga amewataka viongozi wa wilaya kuweka utaratibu mzuri wa kuonesha fedha zilizotekeleza miradi zimetoka wapi kama ni UVIKO 19,tozo au fedha za ndani hii itasaidia wananchi kuelewa matumizi ya mapato katika wilaya yao.
“tuwatie moyo katika shughuli wanazofanya lakini pili tuwe na report kamili kubadika hapo taarifa watahamisika kuelewa matumizi ndio uwazi na ukweli” ameongeza Dr Nyamahanga
Mkuu wa mkoa Mh.Queen Sendiga amemuondoa shaka mwenyekiti wa kamati ya siasa juu ya utekelezaji wa ilani ya chama katika mkoa na miradi yote imetekelezwa kulingana na maelekezo ya chama kwa serikali.
Mh.queen Sendiga ametumia wakati huu wa kukabidhi miradi kushukuru viongozi wote na mashirika yote ambayo ameshirikiana nao katika kutekeleza miradi hiyo kwa muda mfupi na kukamilika katika ubora na kiwango kizuri.
“naomba niwashukuru wajumbe wenzangu wa kamati ya siasa na kipekee niishukuru timu yangu ya mkoa wakuu wa vitengo, viongozi wa taasisi TARURA, TANESCO na IRUWASA hakika ushirikiano wenu ndio umefanikisha haya yote “ amesema Mh Queen Sendiga
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.