Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe: Queen Cuthbert Sendiga amezindua matumizi ya App ya Nikonekt ambayo inamwezesha mwananchi kuunganishiwa umeme kidigitali.
“Napenda kutoa pongezi kwa Tanesco mkoani Iringa kwa kuwajali wananchi wake na kuwarahisishia huduma zaidi kwa kuwapa nafasi ya kuunganishiwa na umeme wakiwa na simu yao kiganjani bila kufika katika ofisi za Tanesco kama ilivokuwa awali.” Mhe:Sendiga.
Licha ya pongezi nyingi alizozitoa Mheshimiwa Sendiga ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza miundombinu ya umeme ili kuepusha gharama zisizokuwa za lazima katika kufanya matengenezo.
Pawaga Road
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, Iringa
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2021, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.