Ameyasema hayo katika kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika tarehe 16/12/2019. Pia amesema zimetengwa kiasi cha Shilingi 18 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa barabara za ndani ambapo TANROADS zimetengwa Shilingi 12 bilioni na TARURA zimetengwa Shilingi 6 bilioni. Umakini unahitajika katika utunzaji wa barabara, kwani vyombo vya Dola vimejipanga katika ulinzi na kukagua uharibufu wa barabara hizi.
Amesema barabara ni moja kati ya eneo muhimu sana katika kujenga uchumi. Sehemu nyingi za wakulima zinategemea mtandao wa barabara kwani baada ya msimu huu wananchi wanategemea kusafirisha bidhaa kwenda kwenye maghala ya kuhifadhia. Kupitia kikao hiki muhimu anatumaini mutaonesha maboresho kati ya TARURA na TANROADS.
Amesema pia, miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mkoa wa Iringa mfano barabara ya Mafinga – Mgololo, barabara ambayo ina uchumi mkubwa sana, uwanja wa ndege wa Nduli ambapo utatanuliwa na kuwezesha safari za ndege kubwa kubwa, pia kuongeza misafara badala ya kwa wiki mara tatu na kuwa siku zote za wiki na ziweze kutua bila shida.
Ameongeza kuwa barabara ya Iringa – Ruaha (Mbuga ya Ruaha) nayo ipo katika hatua za mwisho za maridhiano na kufanya tathmini ya malipo ya fidia kwa wananchi n.k. Barabara ya Iringa – Kilolo nayo ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo na tenda itatangazwa muda si mrefu.
Amemshuruku Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa kuongeza zawadi katika Mkoa wa Iringa ni matumaini kuwa uchumi utaongezeka sana, hata ndege za mizigo zitaanza kutua Mkoani Iringa.
Amehitimisha kwa kusema, nawaagiza Manispaa ya Iringa mji mzima uwe na taa za barabarani ili kuwe na usalama wakati wa usiku. Pia ziainishwe barabara zote.
mbovu zitengewe bajeti na zifanyiwe ukarabati, siyo vema kuwatoza wananchi pesa kwa ajili ya matengenezo ya barabara.
Imetolewa na Ofisi ya Habari Mkoa,
Humphrey Kisika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.