Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Queen Sendiga amewaasa wananchi wa Mkoa wa IRinga kujijengea tabia ya kulinda miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika maeneo yao.
Ameyasema hayo wakati akifanya ziara ya kukagua ujenzi wa bwawa(Rambo) la kunyweshea mifugo katika kijiji cha Kitelewasi, kata ya Mbalamaziwa wilayani Mufindi, ambalo limejengwa kwa na mfuko wa kunusuru kaya maskini )TASAF).
“kwasababu tumefanya kazi kubwa sana kwenye kuchimba hili bwawa jamani na limekaa vizuri baasi tulilinde, tuweke ulinzi miongoni mwetu, ikibidi hata kwenye bwawa hili tutengeneze kamati yetu ya ulinzi” Mhe.Queen Sendiga.
AidhaMkuu wa Mkoa amewaasa wananchi kuendelea kulinda vyanzo vya maji kwa dhumuni la kujihakikishia upatikanaji wa maji hayo ya kunywesha mifugo kwa muda wote.
Nae mkuu wa wilaya ya Mufindi Mhe.Saad Mtambule amepongeza juhudi ambazo zinafanywa na serikali kwa wananchi wake kwani uwepo wa bwawa hilo utasaidia wananchi kunywesha mifugo yao vizuri na kuondoa kabisa kero ambayo wananchi walikua wanakutana nayo hapo awali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.