Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt . Doto M. Biteko amewataka Wanamichezo Kutumia Nafasi Zao Katika Kutangaza Vivutio vya Utalii Ndani ya Nchi na Nje ya Nchi na kulinda Mazingira kwa Kuwaelekeza Watu Umuhimu wa Utunzaji wa Mazingira.
Ameyasema hayo leo October 04,2023 Katika Viwanja Vya Samora Mkoani Iringa Wakati Akifungua Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Ambapo Amewataka Washiriki wa Michezo Hiyo Kutangaza Vivutio Mbalimbali vya Utalii Vilivyopo Nchini Tanzania Ili Kukuza Uchumi Katika Taifa na kupelekea Sekta ya Utalii Kukua kwa Kasi kubwa.
Aidha Mhe. Dkt. Biteko amewasisitiza Wanamichezo hao kuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa Mazingira katika kupanda Miti kulinda na vyanzo vya Maji, Amesema kuwa haita pendeza sana kuona wanamichezo ambao ni watumishi wa serikali wanakuwa watu wa kwanza kuharibu mazingira.
Nae Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Patrobas Katambi (MB) ametoa shukrani kwa serikali kwa kuanzisha mashindano hayo ambapo pia amesema kuwa hii ni Michezo ya 37 tangu kuanzishwa kwake huku Watumishi 2765 wameshiriki katika michezo hiyo vikiwemo na vilabu 68 kwa mwaka uhu 2023.
Akitoa taarifa ya mkoa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima O. Dendego ameishukuru serikali ya awamu ya SITA (6) kwa kazi kubwa inayofanya Katika mkoa huo kwa Kuleta Miradi mingi ya Maendeleo pia kwa Kuruhusu mwaka huu mashindano ya SHIMIWI kufanyika mkoani hapa Kwani mashindano haya yamechangia na Kuongeza kipato na uchumi wa mkoa hapa. Mashindano haya ya Shimiwi yanatarajiwa Kufungwa siku ya tarehe 14/10/2023 Mkoani Iringa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.