Baada ya Ufunguzi wa Maonyesho ya Utalii Karibu Kusini Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima O. Dendego amewaongoza viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya Viongozi wa Kitaifa toka Wizara tofauti tofauti na Wananchi wa Mkoa wa Iringa katika utalii wa matembezi ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mkoani humo.
Katika matembezi hayo Mhe. Halima Dendego amewataka wananchi na viongozi wote kutunza vivutio vinavyopatikana katika Mkoa wa Iringa akisema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha Inaboresha miundombinu katika sehemu zote zenye vivutio vya utalii kwa Lengo la kukuza sekta ya Utalii na Kuvutia Wawekezaji ili kukuza Uchumi wa Taifa.
Akiwa katika matembezi Hayo Mkuu wa Mkoa Mhe. Dendego ametembelea katika Jiwe Linaloongea lijulikanalo kama jiwe Gangilonga, Iringa Boma,Kitanzini, Kalenga na Ismila.
Maonyesho ya Utalii Karibu Kusini Mwaka 2022 yanafanyika katika Mkoa wa Iringa Viwanja vya Kihesa Kilolo yakihusisha Mikoa Kumi Iliyopo Kusini.
Imetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.