Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, leo amefungua Kongamano la Wahariri wa habari na Wadau wa Uhifadhi wa Mazingira na Utunzaji wa Vyanzo vya Maji lililofanyika katika Ukumbi wa Masiti uliopo Mkoani Iringa.
Akifungua Kongamano hilo Mhe. Mpango amesema kuwa kwa sasa kiwango cha Uharibifu wa Mazingira kimeongezeka kwa kiasi kikubwa hivyo kwa wale wote ambao wamezuia Maji yasiende kwenye mto mkuu wa Ruaha na badala yake wamechepusha maji hayo kwenda kwenye mashamba yao wachukuliwe hatua kali ikiwa kubomoa vizuizi ( kuta) hizo tena kwa ghalama zao kwa wote waliohusika na uharibifu huo na bila kujali vyeo vyao. Hivyo nawaagiza Mamlaka bonde kusimamia agizi hilo kuanzia leo, Pia naiagiza wizara husika kukagua vibali vyote vilivyotolewa na baada ya ukaguzi huo nataka vibali vyote viletwe ofisini kwangu.
" Ndugu zangu najua hii vita siyo ndogo ila nitambana nayo maana awezekani hizo Familia 12 ndio zilete janga hili kubwa kwa Taifa wakati wao wakiishi maisha ya starehe.
" Inashangaza sana kuona makundi makubwa ya mifugo yanaingizwa kwenye hifadhi zetu kwa makusudi kabisa na wapo viongozi au askari wanachukua rushwa na mamlaka zipo, naagiza vyombo vichukue hatua ili tujue hii mifugo ya nani"
Akitoa taarifa ya Mkoa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima O. Dendego amesema kuwa katika suala la kutunza mazingira Mkoa wa Iringa ni wa pili kitaifa, na sisi kama Mkoa tumejiweke malengo ya kupanda miti kwa mwaka wastani wanapanda miti takribani Millioni Thelathini.
Imetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.