Halmashauri ya mji wa Mafinga imetumia maonesho ya Nanenane kujifunza fursa zinazoweza kuwanufaisha wananchi wa Mafinga.
Kauli hiyo ilitolewa na mkurugenzi wa mji wa Mafinga, Saada Mwaruka alipokuwa akielelezea umuhimu wa Halmashauri yake kushiriki katika maonesho ya Nanenane mjini Mbeya jana.
Mwaruka alisema “ushiriki wa Halmashauri ya mji wa Mafinga katika maonesho ya Nanenane ni fursa ya kubaini na kujifunza fursa mbalimbali za kilimo, mifugo na uvuvi ambazo zitaweza kuwanufaisha wananchi wetu”.
Akiongelea fursa za kilimo zilizopo katika Halmashauri ya Mji Mafinga, mkurugenzi huyo alisema kuwa Halmashauri yake inayo maeneo mazuri yanayofaa kwa ajili ya kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na bustani. Aliyataja mazao yanayolimwa kuwa ni mahindi, alizeti na maharage. Fursa nyingine alizitaja kuwa ni ufugaji wa ng’ombe, kuku na mifugo mingine.
Mwaruka alisema kuwa Halmashauri yake yenye hekta zaidi ya 64,000 zinazofaa kwa kilimo imejipanga kuongeza uzalishaji na tija ili kufikia uchumi wa kati. Maonesho ya shughuli za wakulima Nanenane mwaka 2017 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi kufikia uchumi wa kati”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.