• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

MAENEO YA UHIFADHI TANZANIA HAYAJAPIMWA

Posted on: February 5th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Tanzania inakabiliwa na changamoto ya uhifadhi wa misitu baada ya maeneo mengi kutokuwa na mipaka inayotambulika rasmi.

Kauli hiyo ilitolewa na waziri wa maliasili na utalii, Dr. Hamis Kigwangala alipokuwa akiongea na kamati ya kitaifa ya ushauri wa misitu katika ukumbi wa chuo cha VETA mjini Iringa jana.

Dr. Kigwangala alisema “kwa muda huu mfupi ambao nimekuwepo hapa katika wizara hii, nimegundua kuwa suala la uhifadhi wa misitu ni jambo lenye changamoto nyingi sana. Na changamoto hizi hasa zinatokana na sisi wenye dhamana ya uhifadhi wa misitu hii kwa maana ya watendaji wa taasisi zetu, na hivyo kutoa mwanya kwa misitu yetu mingi kuvamiwa na wananchi” alisema Dr. Kigwangala.

Alisema kuwa wizara yake inaendelea kutekeleza maagizo ya waziri mkuu ya kuweka alama katika misitu yote ili wananchi wapate kuitambua na kuiheshimu. Vilevile, alikemea tabia ya baadhi ya wananchi kugomea zoezi hilo na maeneo mengine kubomoa alama hizo baada ya kuwekwa na wataalamu. Aliwataka wananchi kuheshimu alama hizo ambao ni mkakati wa serikali kumaliza migogoro ya wananchi kuvamia maeneo yaliyohifadhiwa iliyodumu kwa muda mrefu.

Katika salamu za mkuu waa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema kuwa wizara imekuwa ikiunga mkono juhudi za kuendeleza utalii kwa Mkoa wa Iringa na mikoa ya nyanda za juu kusini.

Mkuu wa Mkoa alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa utalii unakuwa endelevu, Mkoa wa Iringa umefanya utalii kuwa agenda ya kudumu katika vikao vyake. Alisema kuwa Mkoa umejipanga kuendeleza eneo la Kihesa kilolo kwa kukuza utalii kwa kulitunza, kuliendeleza na kulihifadhi. Utunzaji wa eneo hilo utachangia uendelevu wa sekta ya utalii na uhifadhi mkoani Iringa na ukanda wa nyanda za juu kusini, alisema mkuu wa Mkoa.

=30=

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA - 2023 December 17, 2022
  • MAADHIMISHO YA KARIBU KUSINI MWAKA 2022 September 19, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KONGAMANO LA FUNDI SMART LAFANYIKA LEO IRINGA .

    March 17, 2023
  • Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima O. Dendego akifungua kikao cha kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika leo tarehe 25/03/2023 katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya İringa

    March 14, 2023
  • TUNATAKA KUONA MAPINDUZI YA KIJANI KATIKA MKOA WA IRINGA: RC DENDEGO

    February 28, 2023
  • FANYENI KAZI KUWAHUDUMIA WANANCHI

    February 21, 2023
  • Tazama zote

Video

UZINDUZI WA ZAHANATI YA ITAGUTWA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Pawaga Road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, Iringa

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2021, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.