• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

KIKAO CHA BARAZA LA BIASHARA LA MKOA WA IRINGA

Posted on: September 6th, 2019

Kikao kilifanyika katika Ukumbi wa Siasa na Kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tarehe 05/09/2019,lengo likiwa ni kujadili changamoto na kutoa maoni nini kifanyike ili kuboresha uwekezaji Mkoani Iringa.

Kikao hiki kimeongozwa na Mhe. Ally Hapi Mkuu wa Mkoa wa Iringa kama Mwenyekiti  na Katibu Tawala wa Mkoa Iringa kama Katibu, pia Mhe. Richard Kasesela Mkuu wa Wilaya ya Iringa kama mwenyeji wa Wilaya. Pia kulikuwa na Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Iringa na Wakurugenzi wote wa Wilaya za Mkoa wa Iringa, wadau wa maendeleo na wafanyabiashara wa Mkoni Iringa na wawakilishi mbalimbali kutoka Wilaya zote.

Taasisi kama TANTRADE, Benki Kuu ya Tanzania, RIFO, TPSF, TCIA pia zilikuwepo ili kujadili changamoto kwa pamoja na kutolea maoni nini kifanyike.

Akitoa utangulizi katika kikao hicho, Mhe. Hapi amesema, Baraza la Biashara la Mkoa wa Iringa ni ustawi wa maendeleo yetu ya Mkoa. Kutokana na kikao hicho kutofanyika kwa muda mrefu, kwani mara ya mwisho kikao kama hicho kilifanyika Septemba, 2017, Mhe. Hapi ametoa maelekezo kuwa kikao hicho kinatakiwa kufanyika mara mbili kwa mwaka.

Kufanyika kwa vikao hivyo kunafanya wafanyabiashara kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa na wajumbe wote, ili kufahamiana na kujadili mipango na mikakati, pia kuona changamoto na kuzijadili kwa pamoja, kwani ni muhimu Serikali kushirikiana na Sekta Binafsi. Changamoto zinazoikabili nchi yetu haziwezi kutatuliwa na Serikali peke yake, hivyo ni muhimu kuwepo na Sekta Binafsi, mfano shule, kilimo, ufugaji n.k. nini kifanyike kutatua changamoto hizi kama Mkoa.

Kuna madini katika Mkoa wetu ambayo yanapatikana sehemu mbalimbali kama Nyakavangala, Ifunda, Mlata lazima iendelezwe ili watu wafanye biashara za madini. Kuwekeza katika Sekta ya viwanda, maziwa, nguzo  ili kuendeleza Mkoa wetu.

Pia kuendeleza vivutio kama Kalenga, Boma, mashamba ya chai ili watalii waingie kwa wingi katika Mkoa wetu. Mikakati mingi imewekwa kama kupanua kikwanja cha ndege,barabara ya kwenda Ruaha, kujenga mahotel ili watalii waupende Mkoa wetu.

Serikali imejipanga vizuri katika uwekezaji, ili kuwavutia watalii na wawekezaji katika kuwapatia ardhi, maji safi na salama, umeme na vyote vinapatikana bila shida na kwa wakati. Pia kuondoa kero zote kwa wawekezaji kama kunyanyaswa, kusumbuliwa, kuombwa rushwa, kutelekezwa na mengine mengi yanayofanana na hayo.

Nimetoa ombi kwa UNDP kwa ajili ya mambo haya:-

  • Kutengeneza Investment Guide
  • Ofisi Maalum kwa ajili ya wataalam
  • Capacity Building

Pia alitoa agizo kwa TANESCO kuwa, kiwanda kikishawekwa mahali ni lazima umeme ufike hapo mara moja. TARURA nao walielekezwa kuhakikisha barabara zinaptika wakati wote wa mwaka, halikadhalika kwa Mamlaka ya Maji Safi na Salama. Pia Taasisi zote wanatakiwa kufahamu Mkoani kwake kuna wawekezaji wangapi/viwanda ili wajipange katika kutoa huduma husika.

Maendeleo ya Viwanda na Changamoto Zake

Taasisi kama Fire, Washer; msigeuke kuwa kero kwa wawekezaji, wanatakiwa kuelimishwa na kupewa ataraibu na sharia. Au kutoa onyo kama kunakuwa na makosa madogomadogo ambayo yanaweza kurekebishika.

Wakaguzi wanapokwenda kukagua viwanda ni lazima wapte kibali kwa Mkuu wa Wilaya husika, na waseme wanaenda kufanya nini. Hata kama ni Jeshi la Polisi wanaenda kumkamata muhalifu lazima Mkuu wa Wilaya ajue na atoe kibali. Ili kila anayetaka kuwekeza aione Iringa  ni mahali salama.

Alimaliza kwa kusema kuwa, mkutano huu ni kwa ajili ya kujadili changamoto na mafanikio (maoni) karibuni sana.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA - 2023 December 17, 2022
  • MAADHIMISHO YA KARIBU KUSINI MWAKA 2022 September 19, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KONGAMANO LA FUNDI SMART LAFANYIKA LEO IRINGA .

    March 17, 2023
  • Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima O. Dendego akifungua kikao cha kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika leo tarehe 25/03/2023 katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya İringa

    March 14, 2023
  • TUNATAKA KUONA MAPINDUZI YA KIJANI KATIKA MKOA WA IRINGA: RC DENDEGO

    February 28, 2023
  • FANYENI KAZI KUWAHUDUMIA WANANCHI

    February 21, 2023
  • Tazama zote

Video

UZINDUZI WA ZAHANATI YA ITAGUTWA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Pawaga Road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, Iringa

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2021, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.