• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

IRINGA DC KUAJIRI WALIMU WA MUDA WA SAYANSI

Posted on: May 24th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Walmashauri ya Wilaya ya Iringa inaajiri walimu wa muda mfupi katika mkakati wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa walimu wa sayansi.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Iringa, Mariam Mlilapi alipokuwa akisoma risala ya utii ya wananchi wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa Rais Dkt John Magufuli wakati Mwenge wa uhuru ulipokuwa Tarafa ya Isimani wilayani Iringa.

Mlilapi alisema kuwa halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina upungufu wa walimu 145 wa masomo ya sayansi. “Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina mahitaji ya walimu 381 wa sayansi, waliopo mpaka sasa ni walimu 236 hivyo kuwa na upungufu wa walimu hao 145” alisema Mlilapi. Jitihada zinazofanyika kupunguza changamoto ya walimu wa masomo ya sayansi ni kuajiri walimu wa muda mfupi wa masomo hayo kupitia fedha za fidia ya ada kipengele cha taaluma, aliongeza Mlilapi.

Akiongelea ufuatiliaji na usimamizi wa mifumo ya ithibati na ubora wa elimu, kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Iringa alisema kuwa halmashauri hiyo imekuwa ikifanya ziara katika shule ili kukagua mambo mbalimbali yanayolenga utekelezaji wa sera ya elimu ya taifa. “Ofisi ya mthibiti ubora wa elimu kwa kushirikiana na halmashauri imekuwa ikifuatilia, kusimamia na kuhakikisha ubora wa elimu unaotolewa shuleni unakidhi vigezo vilivyowekwa na serikali, ambapo jumla ya shule za sekondari 15 kati ya 36, shule za msingi 85, kati ya 149 na chuo kimoja cha ualimu zimekaguliwa katika kipindi cha Januari-Mei, 2018” alisema Mlilapi.

Mwenge wa uhuru ukiwa katika halmashauri ya Wilaya ya Iringa umekimbizwa umbali wa Km 218 katika Vijiji saba, Kata saba na Tarafa nne.

Ikumbukwe kuwa halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina wakazi 254,032 kwa mujibu wa sense ya mwaka 2012, wanaume wakiwa 123,243 na wanawake 130,789. Tarafa sita, Kata 28, Vijiji 133, Vitongoji 747 na Kaya 60,160.

=30=


Matangazo

  • BURIANI HAYATI RAIS JOHN POMBE MAGUFULI March 19, 2021
  • Ratiba ya Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa Mwezi Machi March 08, 2019
  • Ratiba ya Mh. Mkuu wa Mkoa kwa Mwezi Aprili April 04, 2019
  • Rc Hapi Aanza Ziara Kukagua Miradi Halmashauri Za Iringa August 27, 2019
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MKUU WA MKOA QUEEN SENDIGA AWATAKA WAKUFUNZI WA MRADI WA SEQUIP KUFWATA KILICHO WALETA .

    June 22, 2022
  • RC SENDIGA AONGOZA KIKAO KAZI CHA KUFANYA TATHIMINI UTENDAJI WA TASAF.

    June 21, 2022
  • CCM MKOA WA IRINGA WANAFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO MKUBWA NA SERIKALI YA MKOA NDIO MAANA KUNAUTULIVU MKUBWA NA KASI KUBWA YA MAENDELEO.

    June 17, 2022
  • SENEDA AWAPONGEZA MAAFISA ELIMU WOTE NDANI YA MKOA WA IRINGA KWA ONGEZEKO LA UFAULU MZURI KITAIFA.

    June 14, 2022
  • Tazama zote

Video

MAFANIKIO YA TARURA NA TANROADS MKOA WA IRINGA YAPAMBA MBOTO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Pawaga Road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, Iringa

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2021, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.