• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

WAKURUGENZI MSM WATAKIWA KUANDAA MPANGO WA KUHIFADHI VYANZO VYA MAJI

Posted on: March 22nd, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa mkoani Iringa watakakiwa kuandaa mpango mkakati wa kuhifadhi maji na vyanzo vyake ili viwe endelevu.

Agizo hilo lilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji kilichofanyika katika kijiji cha Mdabulo wilayani Mufindi leo.

Kufuatia uharibifu wa maji na vyanzo vyake kuendelea katika mamlaka za serikali za mitaa, Masenza aliwaagiza wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kuandaa na kuwasilisha mpango mkakati wa utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji mkoani Iringa. Alisema kuwa maji ni muhimu kwa maisha ya wananchi hivyo, vyanzo vyake vinatakiwa kulindwa ili viwe endelevu. Vilevile, aliwataka kutumia sheria ya maji katika usimamizi na uhifadhi wa vyanzo vya maji katika maeneo yao.

Aliwataka pia kusimamia mikataba na miradi ya maji ili iwe vizuri. Alisema kuwa usimamizi mzuri wa mikataba ya miradi ya maji utasaidia kupunguza migogoro baina ya wakandarasi na serikali.

Wakati huohuo, mkuu wa mkoa wa Iringa alimtaka mhandisi wa maji wa mkoa kuandaa na kuwasilisha mkakati wa kuanzisha jumuiya za watumia maji katika wilaya zote mkoani Iringa. Alisema kuwa jumuiya za watumia maji zina mchango mkubwa katika usimamizi wa rasirimali maji katika mamlaka za serikali za mitaa.

=30=




Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC SERUKAMBA AMESHIRIKI NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA MDOGO WAKE NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU MHE WILLIAM LUKUVI

    June 07, 2025
  • WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA

    June 06, 2025
  • MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA KITAIFA YATAFANYIKA MKOA WA IRINGA

    June 02, 2025
  • KAMBI YA MADAKTARI BINGWA YA MAMA SAMIA YATUA IRINGA

    June 02, 2025
  • Tazama zote

Video

WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.