Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego leo 25/10/2023 amefanya ziara ya kutembelea Miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambapo ametembelea Zahanati ya Kijiji cha Mwambao Kata ya Ulanda Tarafa ya Kalenga na Kupongeza ujenzi wa zahanati hiyo huku akiahidi kuchangia Magodoro matatu kwa wwahudumu watakaoletwa na serikali katika kituo hicho
Akiwa katika zahanati hiyo pia Dendego ametoa shukrani nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluh Hassan kwa Kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha watanzania huduma zinawafikia potepote pale walipo
Sambamba na hayo Mhe. Dendego amesikiliza kero za wananchi na baadhi ya hizo kero kuzitolea majibu na zingine akiahidi kuzitekeleza hapo baadae