Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) wametoa semina kwa watumishi wa umma waliopo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Manispaa ya Iringa ikiwa na lengo la kuelezea umuhimu wa mawasiliano na changamoto zake.
Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Siasa ni kilimo huku Meneja wa TCRA nyanda za juu kusini Mhandisi Asajile John akiwataka watumishi hao kutumia Teknolojia ya mawasiliano vizuri kwani endapo watatumia vizuri watapata fursa nyingi kupitia teknolojia hiyo.
Hata hivyo baadhi ya washiriki walioudhuria katika semina hiyo wameupongeza uongozi wa TCRA kwa kuwapatia semina hiyo wakisema kuwa kupitia semina hiyo wamejifunza mambo mengi ikiwemo baadhi ya vitu ambavyo vimekuwa vikifanywa na watu wengi wakidhani ni sahihi kumbe ni makosa.
Hata hivyo semina hiyo imeudhuriwa na baadhi ya viongozi akiwemo Mhe, Mohamed Moyo, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Ndugu Deogratias Hinza, kaimu katibu Tawala sehemu ya Utawala na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa.
Imetolewa na Afisa Habari Mkoa wa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.