• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

SERIKALI YATOA MASHARTI MATATU KUFUNGULIWA MGODI WA NYAKAVANGALA

Posted on: February 20th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Serikali yatoa masharti matatu kufungua mgodi wa kuzalisha dhahabu Nyakavangala na kuelekeza yatekelezwe ndani ya wiki mbili.

Masharti hayo ambayo ni kupitisha kanuni za uchimbaji madini, wataalam kutoka wizara ya madini kukagua mashimo yote ya kuchimba dhahabu na mafunzo ya usalama katika machimbo yalitolewa na naibu waziri wa Madini, Dotto Biteko aliyefanya ziara ya siku moja katika mgodi wa Nyakavangala uliopo katika Kata ya Malengamakali wilayani Iringa jana.

Biteko alisema kabla ya kufunguliwa mgodi huo mambo hayo matatu lazima yafanyiwe kazi ili kufanya mazingira ya uchimbaji dhahabu kuwa salama. Katika kuhakikisha mazingira yanakuwa sawa, aliwataka wachimbaji hao kuwa wakweli na wazalengo kwa nchi yao katika kiasi cha dhahabu kinachozalishwa mgodini hapo. Akiongelea utoroshaji madini hayo, alisema “mchimbaji anayedhani serikali ya Dr. John Magufuli anaweza kutorosha dhahabu atafute kazi nyingine” alisema Biteko. Aliongeza kuwa serikali ipo makini kuhakikisha madini hayo yanawanufaisha watanzania na kuchangia katika uchumi wa Taifa.

Awali mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema kuwa katika kuhakikisha hali ya machimbo dhahabu ya Nyakavangala inakuwa salama, kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Iringa iliagiza ufanyike ukaguzi katika mashimo yote yanayochimba dhahabu katika mgodi huo. Alisema lengo la ukaguzi huo ni kuwahakikishia usalama wachimbaji hao na kuepuka vifo vitokanavyo na mashimo hayo kuanguka.

=30=

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC SERUKAMBA AMESHIRIKI NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA MDOGO WAKE NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU MHE WILLIAM LUKUVI

    June 07, 2025
  • WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA

    June 06, 2025
  • MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA KITAIFA YATAFANYIKA MKOA WA IRINGA

    June 02, 2025
  • KAMBI YA MADAKTARI BINGWA YA MAMA SAMIA YATUA IRINGA

    June 02, 2025
  • Tazama zote

Video

WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.