• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

SERIKALI KUWEZESHA VIJANA KUKOPA

Posted on: March 1st, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya mikopo ili waweze kujiajiri kupitia viwanda.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hotuba yake ya uzinduzi wa kongamano la kuhamasisha vijana kushiriki ujenzi wa Tanzania ya viwanda lililofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa jana.

Masenza alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa vijana na imetengeneza mazingira mazuri ya uwezeshaji mikopo yenye riba nafuu kwa vijana. Alisema kuwa uwezeshaji huo hufanyika kupitia mifuko mbalimbali ukiwemo, mfuko wa maendeleo ya vijana ambao upo halmashauri na mfuko wa wajasiriamali ambao upo SIDO. “Hivyo, nitoe rai kuwa mifuko hii itakuwa ni kichocheo na chanzo mojawapo ya mitaji kwa vijana ya kuanzishia viwanda Vidogo” alisema Masenza.

Akiongelea uwekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo, mkuu wa mkoa alisema kuwa mkoa una hali nzuri ya hewa inayoruhusu ustawi wa mazao ya aina mbalimbali ya chakula na biashara. Alisema kuwa mkoa una fursa za uwekezaji katika viwanda vya usindikaji wa matunda, mbogamboga, mazao ya nafaka na mafuta. Vingine ni viwanda vya kusindika maziwa, nyama na vyakula vya mifugo. Uwekezaji mwingine aliutaja kuwa katika viwanda vya kutengeneza zana za kilimo kama mashine za kuvunia mazao ya mpunga, mahindi na kupukuchua mahindi.

Kongamano la kuhamasisha vijana kujiingiza katika shughuli za uzalishaji katika sekta viwanda na biashara na uzinduzi wa kampeni yenye kaulimbiu ya ‘kijana hamasika, shiriki kikamilifu kuiunda Tanzania ya viwanda’.

=30=



Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC SERUKAMBA AMESHIRIKI NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA MDOGO WAKE NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU MHE WILLIAM LUKUVI

    June 07, 2025
  • WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA

    June 06, 2025
  • MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA KITAIFA YATAFANYIKA MKOA WA IRINGA

    June 02, 2025
  • KAMBI YA MADAKTARI BINGWA YA MAMA SAMIA YATUA IRINGA

    June 02, 2025
  • Tazama zote

Video

WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.