Katika kuendeleza sekta ya kilimo nchini Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ameishauri Halmashauri ya Mji Mafinga katika moja ya miradi yake ya umwagiliaji, kuwekeza katika kilimo cha vitunguu.
Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua Miradi iliyopo katika Halmashauri hiyo
Akiwa katika Mradi huo wa Umwagiliaji wa Mtula unaosimamiwa na Tume ya Umwagiliaji, uliopo katika kata ya Sao Hill Mhe. Serukamba amesema kuwa ni lazima thamani ya Mradi iendane na thamani ya mazao ambapo amewashauri wananchi na Halmashauri hiyo katika kipindi hiki kulima zao la kitunguu ambalo kwa sasa lina soko kubwa
Pia Mhe. Serukamba ameongeza kwa kusema kuwa kupitia zao hilo la vitunguu Pato la wananchi wa eneo hilo litaongezeka na uchumi wa eneo hilo utakuwa kwa kasi kwani watu hawatataja eneo lingine zaidi ya Mtula
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe.Dkt. Linda Salekwa ametoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa kwa kuja na wazo zuri na wao wamelichukua na kama Mkuu kiongozi amesema ataanza kulifanyia kazi kwa kuhakikisha wananchi hao wanapata Elimu juu ya zao hilo la vitungu.
Pia Mhe. Salekwa amesema kuwa katika eneo hilo lenye ekali 76 mbali na kulima zao hilo la vitunguu lakini tayari wamekwisha kutenga maeneo ya kulima mboga mboga kwa lengo la kutokomeza udumavu.
Nae Meneja wa Mradi huo Mhandisi Peter Akonaay amesema kuwa ujenzi wa mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 98 umegharimu zaidi ya Millioni Mia Tano na utanufaisha kaya 46 ambapo ni sawa na watu 131.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.