Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh:Queen Cuthbert Sendiga leo ameshiriki kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Iringa, kwa lengo la kujadili mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya barabara, changamoto na jinsi ya kuzitatua changamoto hizo.
Mh: Sendiga ameishukuru serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya bilioni 31 za kitanzania kwaajili ya ukarabati, matengenezo na ujenzi wa barabara katika Mkoa wa Iringa.
Na ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kulingana na fedha iliyotolewa amewataka wakuu wa wilaya za mkoa wa Iringa kufanya ufatiliaji wa kina katika utekelezaji wa miradi iliyopo katika maeneo yao.
Aidha amewaomba wajumbe kuwa mabalozi wa barabara kwa wananchi ili wajue kuwa maeneo ya barabara yanatakiwa kutunzwa vizuri "kwahiyo wote tukawe mabalozi ili utunzaji mzuri wa barabara uweze kufanyika tukatoe elimu kwa wananchi ili waweze kujua maeneo yetu yanatakiwa kutunzwa vizuri na watambue kunasheria mbalimbali za uhifadhi wa barabara" RC Sendiga
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.