Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe.Queen Cuthbert Sendiga ametoa pongezi hizo wakati akifunga mafunzo ya wakufunzi wa sensa ya watu na makazi ya waka 2022 katika ngazi ya Mkoa yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu Mkwawa.
Licha ya kuwapongeza Mhe. Queen Sendiga amewataka wakufunzi kila wakati kukumbuka kuwa wana dhima kubwa kwa wananchi na maendeleo ya mkoa wa Iringa halikadhalika maendeleo ya nchi kwa ujumla kwa kuwa Sensa ndiyo msingi wa maendeleo.
“Sina shaka yoyote kuhusu uwezo wenu kwani mmeudhihirisha katika mafunzo haya na ndio maana nimetaarifiwa kuwa hakuna mshiriki aliyeshindwa kuhitimu kwa sababu za kushindwa mitihani.” Mhe. Sendiga
Aidha Mhe. Sendiga ametoa wito kwa viongozi wote pamoja na watendaji wa serikali mkoani Iringa kuhakikisha tunaendelea kutoa elimu kila fursa inapotokea, iwe katika mikutano maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya sensa au mikutano yoyote inayotukutanisha na wananchi na wadau wengine.
“Kila mmoja wetu ana jukumu la kutekeleza ili kufanikisha Sensa. Viongozi wa Serikali, Waheshimiwa Wabunge, Waheshimiwa Madiwani, viongozi wa Serikali za Mitaa, viongozi wa dini, viongozi wa Kisiasa, viongozi wa kijamii na wengine sote tushirikiane kutoa elimu ili kulifanikisha jambo letu hili.” Mhe. Sendiga
Mkuu wa Mkoa wa Iringa pia amesema kuwa Sensa lazima ifanyike na ifanyike kama ilivyopangwa kwa kufuata taratibu na miongozo yote inayopaswa kufuatwa ili kuhakikisha ubora wa taarifa zitakazokusanywa katika mkoa wa Iringa.
“Katika vitu ambavyo wananchi wa mkoa wa Iringa tunapaswa kuvifanya kwa weledi, umakini mkubwa na kwa ubora wa hali ya juu ni pamoja na kufanikisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.” Mhe. Sendiga
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.