Mhe Ally Hapi, Mkuu wa Mkoa Iringa, amefanya ziara ya kutembelea Tarafa ya Idodi na Kata ya Nzihi na kujionea uharibifu uliofanywa kutoka na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Iringa.
Akiwa katika Ziara hiyo Mhe Ally Hapi, alianza kujionea daraja la Nzihi amabalo limebomoka kingo za pembeni mwa daraja hilo na kupelekea kuatarisha maisha ya wasafiri wanatumia njia hiyo, hivyo magari yote yanapita upande mmoja, lakini hata sasa Tanroads wapo kazini kwa ajili ya kutengeneza kingo hizo ili kuzuia daraja hilo lisibomoke.
Baadae Mhe Hapi, na kamati ya Ulinzi na Usalama waliekea katika kituo cha Afya Idodi kwenda kumfariji Bi, Akhadija Keyela, Mkazi wa Kitisi ambaye amefiwa na watoto wake 2 wa kiume ambaye ni Bosko Keyele (8) na Stivini Keyele (5) watoto hao walisombwa na maji wakiwa shambani na mama yao aliyekuwa akiangalia mazao yake. Bi, Akhadija alikuwa na watoto wake 4 shambani ambapo watoto 2 aliwaokoa.
Akiwa Idodi alienda kijiji cha Tungamalenga ambapo aliona uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara pamoja na daraja linalounganisha mbuga ya Ruaha National Park na kijiji cha Tungamalenga. Na baadae alishiriki katika zoezi la ugawaji wa vifaa kwa wahanga waliokumbwa na mafuriko Idodi, msaada huo umetolewa na Redcross pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wenye thamani ya Milion 4,116,500, vifaa hivyo ni magodoro 30,unga kilo 200, maharage kilo 100, blanket 30, ndoo za lita ishirini 15, madumu ya lita ishirini 15, vifaa vya akina mama 15, vifaa vya jikoni 15.
Mhe Hapi, akiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Idodi, amewataka wa Nchi wote wa mkoa wa iringa kuchukua tahadhari na mvua zinazoendela kunyesha, “ amesema kwa mujibu wa taarifa za mamlaka ya hali ya hewa mvua zinazotarajiwa kunyesha ni kubwa sana” hivyo ni vema wananchi wakachukua taadhari mapema. Amewataka wale wote waliojenga mabondeni kuhama haraka sana, walioko mashambani pia nao wasiende kwa kipindi hiki maana hali ya hewa si nzuri sana, na wazazi kuwa makini na watoto wao hasa wanapoenda shule na kurudi majumbani wawafatilie ili wasije wakasombwa na maji, lakini pia amewaonya na walevi wa ulanzi kuwa makini kipindi hiki cha mvua wanywee majumbani au kuacha kabisa na amewataka Wananchi wote wa Mkoa wa Iringa hususani waliokumbwa na mafuriko wachemshe maji ya kunywa ili kuepukana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Imetolwa na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
Humphrey Kisika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.