Mkuu wa mkoa wa iringa Mhe. Peter Serukamba amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Kumuhamisha mara moja Mtendaji wa Kata ya Mkimbizi Bw. Mlole Ngwada baada ya kuingilia eneo la shule na kuanza kufanya shughuli za kilimo
Hayo yamejiri Machi 14,2025 wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa eneo la shule ya msingi Igeleke iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Baada ya ukaguzi wa mipaka ya eneo hilo lenye viwanja 11 ambalo lilitolewa na mmoja wa wanafamilia kisha miaka mitano iliyopita Ndg. Ngwada alianza kufanya shughili za kilimo kwa kumega eneo moja na kudai eneo hilo ni la familia na halikutolewa wakati ule.
Jambo hilo la kuanza kufanya shughuli za kilimo katika eneo la shule lilipelekea wananchi wa eneo hilo kuanza kuhoji juu ya shughuli zinazoendelea na kupelekea Ndg. Ngwada kuanza kutoa vitisho kwa Mwalimu Mkuu wa Shule Hiyo Bi. Victoria Kalinga
Baada ya Mhe. Serukamba kulipitia eneo hilo akatoa maagizo na kusema kuanzia sasa eneo hilo ni la shule na sio la familia lakini pia hakuna kumuhamishwa Mwalimu Mkuu huyo na badala yake ahamishwe mtendaji wa kata hiyo.
Sambamba na hayo serukamba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashuri ya Manispaa ya Iringa kuandaa Hati ya eneo hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.