Waziri wa utalii Mhe, Daktari balozi Pindi chana, Leo tarehe 9/11/2022 amezindua maonyoshe ya utalii Karibu Kusini ya mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Kihesa kilolo katika Manispaa ya Iringa.
Katika uzinduzi huo Waziri Mhe. Pindi Chana, amesema kuwa Mikoa ya kusini imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii hivyo wananchi wanatakiwa kutunza mazingira na hifadhi ili kuendelea kukuza utalii na kuvutia wawekezaji wengi kusini.
" tunaposema utalii lazima tukumbushane kwamba vipo vitu haviendani na vitendo na masharti ya utalii, maswala haya ni pamoja na changamoto ya uchomaji moto hovyo kwenye hifadhi na vivutio vyetu vya utalii hivyo tunapotangaza utalii na kutunza misitu eneo hili la moto lazima tulidhibiti hivi karibuni mtakumbuka tumepata changamoto ya moto huko Kilimanjaro lazima watanzania wote tuungane kusema moto hapana.
Pia Mhe. Pindi Chana, ametoa pongezi kwa Mhe, Halima Dendego kwa maandalizi mazuri ya maonesho hayo karibu Kusini kwani yamefana sana.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima O. Dendego ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha Utalii na kuleta watalii wengi kupitia sinema ya The Royal Tour.
Maonyesho haya yanafanyika kwa muda wa siku Tano yakihusisha Mikoa 10 kutoka kusini mwa Tanzania.
Imetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.