• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

IRINGA WATAKIWA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA

Posted on: November 17th, 2017

IRINGA WATAKIWA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA

Na. Dennis Gondwe, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa -IRINGA

Wananchi wa mkoa wa Iringa wametakiwa kujiunga na mfuko wa Taifa wa bima ya afya ili waweze kunufaika na matibabu bila malipo pindi wanapougua. Kauli hiyo iliyolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza alipokuwa akiongea katika kipindi moja kwa moja cha Nyota ya asubuhi kinachorushwa na kituo cha redio Furaha cha mjini Iringa leo.

Mheshimiwa Masenza alisema “ombi langu kwa wananchi wa mkoa wa Iringa, tuendelee kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili tuendelee kutibiwa bila bugdha”. Alisema kuwa matibabu ni gharama kubwa ila kwa mwananchi aliyejiandaa vizuri, hawezi kupata tatizo la gharama ya matibabu pindi anapougua. Alisema kuwa bima ya afya ni mkombozi kwa wananchi wa kawaida ambao wanapougua hujikuta hawana fedha za kugharamia matibabu.

Aidha, alishauri wananchi hao kuwakatia bima watoto kwa gharma ya Tshs 54,000 ambayo itamuwezesha kutibiwa bure. Alisema kuwa bima ya watoto ni muhimu kwa sababu watoto wengi ni wahanga wa magonjwa kwa sababu kinga yao ya mwili haijaimarika vizuri. “Bima ya watoto kwa Tshs 54,000 itawawezesha watoto kutibiwa sehemu mbalimbali bila gharama” alisema mheshimiwa Masenza.

Akiongelea kampeni ya kupima afya “Afya check campaign” Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dr Faith Kundy alisema kuwa Manispaa ya Iringa itakuwa mwenyeji wa kampeni ya kupima afya  itakayozinduliwa kesho na mkuu wa mkoa wa Iringa, Mheshimiwa Amina Masenza katika uwanja wa bustani ya Manispaa (Garden) kwa lengo la kuwapatia fursa wananchi wa Manispaa kupima hali ya afya zao bure. Alisema kuwa katika kampeni hiyo magonjwa yasiyo ya kuambukiza na magonjwa ya kuambukiza yatapimwa bure. Kampeni ya kupima afya itakwenda sambamba na ugunduzi wa kifua kikuu ngazi ya jamii.

=30=



Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC SERUKAMBA AMESHIRIKI NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA MDOGO WAKE NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU MHE WILLIAM LUKUVI

    June 07, 2025
  • WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA

    June 06, 2025
  • MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA KITAIFA YATAFANYIKA MKOA WA IRINGA

    June 02, 2025
  • KAMBI YA MADAKTARI BINGWA YA MAMA SAMIA YATUA IRINGA

    June 02, 2025
  • Tazama zote

Video

WASHIRIKI 10,000 KUTIKISA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 MKOANI IRINGA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.