Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa katika kufunga mafunzo ya Oparesheni ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT katika Kikosi 841 JK Mafinga na kuwataka wahitimu kuwa wazalendo kwa Taifa.
Akizungumza katika mahafali hiyo Komred Kheri James amelipongeza Jeshi la kujenga Taifa kwa kuendelea kuwa msingi wa malezi na makuzi ya vijana nchini kwa kwa kuwaandaa vijana kuwa na Uadilifu, Utii, Uhodari na kuwajengea uwezo wa stadi za maisha ili kuweza kupata ujuzi wa kujitegemea na kujiandaa kuzifikia ndoto zao.
Akizungumza kwa niaba ya kikosi Kaimu Kamanda wa kikosi Meja Nehemia Japhet Mbwilo amewashukuru wazazi na walezi wa wahitimu wote na ameeleza kuwa ni vyema wahitimu wakayatumia vizuri mafunzo waliopata, ili kutimiza moja ya lengo la Taifa kuwa andaa kuwa jeshi la akiba na kamwe wasiyatumie kinyume cha lengo kwani kufanya hivyo ni usaliti kwa Taifa letu lililotumia gharama kubwa kuwaandaa.
Mahafali hiyo pia ilihudhuriwa na Muwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Meja Jenerali Kahama Juni Mziray, Muwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Kanal Projest Christopher Rutahiwa, wajumbe wa kamati ya usalama, Viongozi, Maafisa, Askari, Wananchi na Wanafunzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.