Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga leo ameongea na vyombo vya habari na kuwataarifu kuwa tarehe 1/7/2022 Mkoa wa Iringa utapokea ugeni wa Makamu wa Rais wa Pili wa Zanzibar na Mwenyekiti mwenza wa kamati kuu ya Sensa Taifa.
Lengo la ujio wa kiongozi huyo ni kufunga mafunzo ya Wakufunzi wa sensa ya watu na makazi waliokuwa yaliyokuwa yakifanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa.
Hivyo Mhe, Sendiga ametumia fursa hiyo kuwalika Wananchi wote wa Mkoa wa Iringa kujitokeza kwa wingi siku hiyo chuoni hapo ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali, muda ni kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Imetolewa na Afisa habari Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2023, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.