|
Maji
Asilimia ya wakazi wa mkoa wa Iringa waliokuwa wakipata huduma ya maji safi na salama ni 54.9%.Asilimia ya wakazi wanapata huduma ya maji safi na salama Desemba 2008 ni 61.2%. Ongezeko la asilimia ya wakazi wanaopata hudumaya maji ni 6.3%.
Idadi ya kamati za maji imeongezeka kutoka 380 mwaka 2005 hadi kufikia 428 Desemba 2008. Mifuko ya maji imeongezeka kutoka Tshs 59,460,220 mwaka 2005 hadi 75,565,569 mwaka 2008. Idadi ya vituo vya kutekea maji vilivyojengwa au kukarabatiwa hadi sasa Desemba 2008 ni 693. Idadi ya wananchi waliohamasishwa kwa njia ya semina shirikishi kuhusu usafi wa mazingira ni 65,054. Wahandisi 5 wameajiliwa na serikali na halmashauri ya Mkoa. Jumuiya ya watumiaji maji zilizosajiliwa kisheria zimeongezeka kutoka 8 mwaka 2005 kufikia 10 mwaka 2008
|