|
|
Huduma za kiuchumi
Mkoa wa Iringa una jumla ya eneo la hekta 58,936,000 kati ya hizo km za mraba 56,864 ni nchi kavu na km za mraba 2,072 ni eneo la maji. Kati ya eneo lote hekta 43,935,000 (74%) linafaa kwa kilimo, ingawa hadi sasa hekta zinazotumika kwa kilimo ni 7,468,950 tu sawa na asilimia 17. Mazao makuu ya biashara na chakula ambayo yanalimwa ni pamoja na Mahindi, Ngano, Pareto, Chai, Viazi mviringo, Matunda, Alizeti, Karanga, Ufuta, Maharage, Nyanya, Mpunga, Tumbaku, Soya, Mtama, Mhogo, Korosho, Artemisia na Paprika.
Eneo linalilimwa mazao mbalimbali limeongezeka kutoka hekta 586,245 mwaka 2005/2006 hadi kufikia hekta 746,895 zilizolimwa msimu wa 2007/2008.Elimu ya kilmo bora ilitolewa kwa wakulima na jumla ya mashamba darasa 750 yalizalishwa na jumla ya wakulima 18,750 wamepatiwa mafunzo kwa vitendo kupitia mashamba haya kwa kipindi cha Desemba 2005 hadi Desemba 2008. Mbolea na nbegu zilizotumika mwaka 2005/2006 zilikuwa tani 12,121 na tani 833 kwa pamoja. Ukilinganisha na tani 45,260 za mbolea na tani 1,125 za mbegu mwaka 2008hii ni sawa na asilimia 53 kwa matumizi ya mbolea na asilimia 26 kwa matumizi ya mbegu.
Uzalishaji wa Mazao makuu ya chakulu na biashara mwaka 2005/2006hadi 2007/2008
| Mazao |
2005/2006 |
2006/2007 |
2007/2008 |
|
Hekta limwa |
Mavuno (Tani) |
Hekta limwa |
Mavuno (Tani) |
Hekta limwa |
Mavuno (Tani) |
| Mahindi |
305,877 |
429,106 |
378,520 |
641,854 |
384,509 |
739,370 |
| Maharage |
56,767 |
49,327 |
73,839 |
58,551 |
68,772 |
83,001 |
| V/Mviringo |
33,750 |
286,289 |
37,194 |
287,973 |
33,177 |
298,455 |
| V/Vitamu |
4,978 |
35,288 |
10,409 |
34,051 |
8,569 |
31,976 |
| Mpunga |
7,238 |
13,842 |
13,538 |
32,001 |
16,693 |
36,032 |
| Ngano |
10,2195,665 |
11,155 |
17,719 |
21,165 |
19,515 |
21,196 |
| Njegere |
5,665 |
9,216 |
11,300 |
11,413 |
6,187 |
22,817 |
| Kunde |
13,079 |
13,588 |
15,009 |
35,053 |
24,710 |
38,936 |
| Karanga |
3,421 |
2,860 |
4,908 |
5,940 |
8,753 |
12,202 |
| Ulezi |
1,308 |
1,109 |
1,276 |
1,453 |
1,662 |
1,941 |
| Jumla |
442,302 |
851,780 |
563,712 |
1,129,454 |
572,547 |
1,285,926 |
Mifugo
Mkoa una jumla ya mifugo ya Mashamba ya mifugo 12 yanayomilikiwa na Serikali na watu binafsi. Mashamba haya huzalisha Maziwa, Mitamba na Madume. Madume haya hutumiwa zaidi na wakulima wadogo kuboresha mifugo yao.
Takwimu za sekta ya Mifugo Mifugo kwa kipindi cha Desemba 2005 hadi Desemba 2008
| Takwimu / Huduma |
Desemba 2005 |
Desemba 2008 |
Ongezeko / Mafanikio |
| Idadi ya Ng'ombe wa kienyeji |
559,597 |
420,187 |
Idadi ya Ng'ombe imepungua kwa 24% baada ya wafugaji kuzingatia wa kibiashara na ubora wake na sio wingi wake. |
| Idadi ya Ng'ombe wa maziwa na nyama (kisasa) |
20,289 |
28,020 |
Idadi imeongezeka kwa 38% |
| Miundo mbinu |
Majosho yaliyokuwepo - 226, yalikarabatiwa - 72 na yaliyotumika 88 |
Majosho yaliyopo - 229, yaliyokarabatiwa - 93 na yaliyotumika 161. |
Majosho yanayofanya kazi yameongezeka yadi kufikia 161 sawa na 82.9% ongezeko hili kubwa ni baada ya selikari kusambaza dawa ya ruzuku. |
| Uzalishaji wa maziwa na nyama |
Maziwa lt 4,592,662, Nyama jumla ya mifugo (n'gombe, kondoo, mbuzi na nguruwe) 62,102walichinjwa N'gombe 26,568 kondoo/mbuzi17,970 na nguruwe 17,564 |
Mazwa lt 6,976,018 Nyama jumla ya mifugo, ( N'gombe, kondoo, mbuza na nguruwe) 72,634 walichinjwa, Ngombe 26,379, kondoo/mbuzi 22,008 na nguruwe 24,247 |
Lita 2,383,356 ikiwa ni ongezeko la 52% |
| Uogeshaji |
Idadi ya miruko ng'ombe 802,220, Mbuzi 107,133, Kondoo 71,372 na Mbwa 10,728. |
Idadi ya miruko Ng;ombe 1,513,056, Mbuzi 404,024, Kondoo 135,121 na Mbwa 26,728 |
Ongezeko la miruko kwa ng;ombe ni 88.6% |
| Zao ngozi |
vipande 16,568 vya ngozi ya ng'ombeviliuzwa. vipande 13,970 vya ngozi ya kondoo/mbuzi viliuzwa |
Vipande 18,375 vya ngozi ya ng'ombe viliuzwa. Vipande 17,970 vya ngozi ya kondoo/mbuzi viliuzwa. |
|
Uboreshaji wa ufugaji wa kuku wa kisasa na kienyeji |
Chanjo ya mdondo - kuku waliochanjwa ni 200,000 |
kuku waliochanjwa kuzuia mdondo ni 1,257,413 |
Ongezeko ni kuku 1,057, 413 sawa na 528.7% hii ni kwa sababu ya matumizi ya dawa ya matone ya i2 sanjari na kampeni ya chanjo kwa kuku wa kienyeji. |
|