THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA - PRIME MINISTERS OFFICE
   
Search the site

 
 .: Home
 .: Organization structure
 .: About Us & Contact
 .: Mission & Vision
 .: Project & Programs
 .: Financial Report & Budget
 .: Documents
Taarifa za idara

 .: Kilimo na Mifugo

.: Maliasili

.: Elimu

.: Afya

.: Maji

.: Ushirika

.: Biashara

.: Barabara na Majengo

.: Ardhi, Upimaji na Ramani

.: Jamii, Jinsia & Watoto

Makundi maalum yaliyoshughulikiwa kati ya Desemba 2005-Desemba 2008 ni kama ifuatayo

Wototo

Mkoa wa Iringa umefanya jitihada mbalimbali katika kusimamia haki na usawa wa watoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na mafanikio yaliopatikana ni kama ifuatavyo:-

  • Watoto 15,452 wanaoishi katika mazingira magumu wametambuliwa na wamepatiwa msaada ya kujikimu ikiwemo mahitaji ya shule (sare na vifaa) mavazi na matibabu.
  • Kamati 240 zimeundwa katika ngazi ya mtaa/kijiji ili kushughurikia matatizo ya watoto walio katika mazingira hatarishi, pia mafunzo yametolewa kwa kamati zote 240 juu ya wajibu wa kamati na malezi ya watoto.
  • Jumla ya Watoto 3,243 wamefaidika na mpango wa ukomeshaji wa ajira mbaya kwa watoto na kujiunga na mafunzo ya ufundi, kuwarejesha shuleni na kuhakikisha wanapata haki zao ikiwa ni pamoja huduma za afya, chakula na mavazi.

Wazee

  • Vikundi saba (7) vya wazee vinavyojishughulisha na shughuli za kiuchumi kama vile kilimo cha mpunga, mahindi, ufugaji wa ng'ombe, mbuzi na kuku wa kienyeji wamepata mtaji wa Tshs. 59,789,366.51 kupitia mradi wa TASAF.
  • Wazee wanapata huduma ya matibabu bure katika hospitali ya Mkoa, Wilaya na katika Zahanati na vituo vya afya vya umma.
  • Kuingiza katika mipango na bajeti shughuli za kusaidia na kuboresha maisha ya wazee kwa kutenga fedha kila mwaka ili kuendesha semina za utambuzi wa haki za Wazee kama zilivyoainishwa kwenye Sara ya taifa ya Wazee, MKUKUTA na mwongozo wa TASAF.

 

opyright © 2009 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, P.O.BOX 858, Iringa, TEL: 026 - 2702715, FAX: 026-2702082 / 2701888

[Go Home]