THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

>
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home About Us Vision & Mission

Vision & Mission

E-mail Print PDF

Dira ya Mkoa

Mkoa ni Taasisi ya Umma inayowezesha na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali ya Serikali kwa wakati na ufanisi wa hali ya juu.

Dhamira ya Mkoa

Kuwa Taasisi yenye wataalamu wenye uwezo na ujuzi unaotosheleza kutoa huduma za ushauri na utaalamu kwa kushirikiana na Wadau wengine wa Maendeleo kwa kuzingatia Sera, Sheria, na Miongozo ya Serikali ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Majukumu ya Mkoa

· Kuziwezesha na kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kutoa huduma zinazohitajika kwa wananchi

· Kuhakikisha huduma bora za kiuchumi na kijamii zinawafikia Wananchi walio wengi kwa ubora na viwango vinavyostahili

· Kuhakikisha amani, usalama na mshikamano unakuwepo Mkoani kwa kuzingatia Utawala Bora

· Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA)

· Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Mipango ya Elimu (MEM, MES), Mpango wa kuendeleza kilimo (ASDP/DADP), Mpango wa Afya na utekelezaji wa miradi yote ya Maendeleo

· Kuhakikisha masuala mtambuka (Ukimwi, Mazingira, Jinsia, nk) yanapewa vipaumbele vinavyostahiki wakati wa kuandaa na kutekeleza Mipango ya Maendeleo.

Mikakati ya Mkoa

Katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 1961 hadi  2010, Serikali ilipanga kutekeleza malengo na mikakati mbalimbali ili kuondoa kero na kuboresha maisha ya Watanzania.

Mikakati hiyo ni pamoja na kutekeleza:-

  • Ilani ya Uchaguzi ya TANU/ CCM ya mwaka 1961 hadi 2010
  • Mkakati wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Miaka Mitano na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, chini ya utaratibu wa mpango wa matumizi wa muda wa kati (MTEF).
  • Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA).
  • Matakwa ya Sera na Sheria zinazosimamia Sekta mbalimbali.
  • Mkakati wa kitaifa wa Kupambana na Kuzuia Rushwa.
  • Sera ya Taifa ya kupambana na UKIMWI.
  • Utekelezaji wa Malengo ya Millinia 2005 – 2010

Katika kuhakikisha mafanikio yanapatikana Mkoa ulijiwekea mikakati ifuatayo:-

a) Kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi yenye ufanisi mkubwa ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

b) Kutengeneza mazingira bora ya Utawala kwa kudumisha amani na umoja.

c) Kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwapatia ushauri wa kitaalamu.

d) Kuhakikisha tunaongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara, kuongeza ubora wa mazao na kuuza kwa bei nzuri na hatimaye kuongeza kipato na pato la Mkoa na Taifa kwa ujumla.

e) Kuhakikisha wadau mbalimbali wanashiriki katika shughuli za Maendeleo.

f) Kuandaa Mipango shirikishi na endelevu.

g) Kuweka mikakati madhubuti ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

 

 

Select Your Language