|
Elimu
Kwa kipindi cha Desemba 2005 hadi Desemba 2008 yamepatikana mafanikio yafuatayo:
- Kuongezeka kwa madarasa ya awali toka 322 hadi 341 sawa na ongezeko la asilimia 5.5
- Kuongezeka kwa wanafunzi toka 25,189 hadi 41,339 ni ongezeko la asilimi 39.
Katika kipindi hiki cha miaka mitatu takwimu zinaonyesha kumekuwa na upungufu wa walimu ya awali kutoka 295 hadi 229 ikiwa ni upungufu wa asilimia 20.
Mafanikio ya kitaaluma kwa elimu ya msingi.
Mkoa umekuwa na maendeleo ya kulidhisha ya utoaji taaluma kwa kutumia kigezo cha matokeo ya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi. Kwa kipindi cha Desemba 2005 hadi Desemba 2008 idadi ya wanafunzi waliofaulu imeongezeka kutoka 27,554 hadi 34,528 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 6,974. Aidha mkoa umetoka nafasi ya 9 kitaifa hadi nafasi ya 3 kama jedwari lifuatalo linavyoonyesha;
| Mwaka-Des |
Waliofaulu |
Waliofaulu |
% |
Nafasi ya kufaulu kitaifa |
| 2006 |
36,040 |
27,554 |
76.5 |
9 |
| 2007 |
42,934 |
29,858 |
69.5 |
3 |
| 2008 |
53,880 |
34,528 |
64.1 |
3 |
Maendeleo haya kitaaluma yamechangiwa na kuongezeka kwa uwiano kati mwalimu na mwanafunzi, vilevile mazingira yakusomea wameboreshwa kwa kuongeza vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na ujenzi wa vyoo.
Mpango wa elimu kwa walioikosa.
Kwa kipindi cha Desemba 2005 hadi 2008 Mkoa uliendelea na jitaihada za kuwapatia nafazi za shule wale watu waliokosa nafasi hiyo ya kawaida katika shule zetu za msingi chini ya mpango unaojulikana kama MEMKWA (Mpango wa Elimu ya Msingi walioikosa). Hadi kufikia Desemba 2008 kulikuwa na wanafunzi 2,411 katika madarasa na vituo 262.
Elimu ya Sekondari
Mwaka 2005 Mkoa ulikuwa na shule za Sekondari zipatazo 135 kati ya shule hizo, shule 102 ni za umma (Region Community and National Secondary Schools) na 33 ni za binafsi (None Govements Secondary School) i.e Seminari, na za watu na mashirika mbalilmbali ya binafsi. Hadi mwaka 2008 Mkoa ulikuwa na shule za sekondari 216 kati ya shule hizo, shule 166 ni za umma na 50 ni za binafsi.
Idadi ya Sekondari Kiwilaya (shule za Serikali - Umma)
| Halmashauri |
Malengo (Shule) kwa kata za Elimu |
Utekelezaji (Shule) hadi 2008 |
Upungufu (Shule) |
Idadi ya mikondo |
| Manispaa |
14 |
9 |
1 |
4 |
16 |
| Iringa (V) |
24 |
21 |
3 |
- |
0 |
| Kilolo |
22 |
20 |
- |
2 |
16 |
| Ludewa |
17 |
17 |
- |
- |
- |
| Makete |
17 |
13 |
1 |
8 |
0 |
| Mufindi |
28 |
40 |
- |
- |
36 |
| Njombe |
28 |
28 |
- |
- |
8 |
| Njombe (M) |
18 |
11 |
1 |
- |
0 |
| Jumla |
166 |
159 |
6 |
14 |
76 |
|