|
Sekta ya Viwanda na Biashara
Sekta ya Viwanda na Biashara inaajiri watu takribani 50,000 hii ikiwa ni sawa na asililma 3.4 ya wakazi 1,590,892 wa Mkoa wa Iringa. Mkoa unazo fursa nyingi zinazoweza kuugeuza Mkoa huu kuwa na Viwanda na kuongeza ajira na pia pato la Mkoa.Nia ya Mkoa nikuhakikisha sehemu kubwa ya mazao yanayolimwa yanasindikwa na kuongezea thamani ili kuinua kipato cha wazalishaji.
Mkoa wa Iringa hadi sasa unavyo Viwanda vya uwekezaji 11 vikubwa, 13 vya kati, vidogo 53 na mashine za kusaga nafaka 1,192.
Mkoa una jumla ya masoko 43 (2008) ikilinganishwa na 24 kuanzia Desemba 2005 ikiwa ni ongezeko la asilimia 44. Lengo la mkoa nikuwa soko katika kila kata.
Idadi ya wajasiliamali waliowezeshwa mafunzo na mitaji
|
2005/2006 |
2006/2007 |
2007/2008 |
| Usindikaji Vyakula |
- |
250 |
230 |
| Uwendeshaji Biashara |
7 |
390 |
805 |
| Ushauri |
150 |
350 |
100 |
| Masoko |
- |
15 |
165 |
| Jumla |
220 |
1,005 |
1303 |
|