THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA - PRIME MINISTERS OFFICE
   
Search the site

 
 .: Home
 .: Organization structure
 .: About Us & Contact
 .: Mission & Vision
 .: Project & Programs
 .: Financial Report & Budget
 .: Documents
Taarifa za idara

 .: Kilimo na Mifugo

.: Maliasili

.: Elimu

.: Afya

.: Maji

.: Ushirika

.: Biashara

.: Barabara na Majengo

.: Ardhi, Upimaji na Ramani

.: Jamii, Jinsia & Watoto

Barabara

Mwaka 2005 Mkoa ulikuwa na mtandao wa barabara upatao km 4,056.15. kati ya hizo km 3,354 ni barabara za vumbi na km 701.90 ni changarawe. Mtandao huo Desemba 2008 umeongezeka hadi kufikia km 6,196.88 kati ya hizo km 511.11 ni lami, km 2454.27 ni changalawe na km 3,230.50 ni barabara ya udongo.

Wakara wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Iringa wanahudumia jumla ya kilometa 1.901.58 zikiwemo za lami km 489.61 na za changarawe km 1,411.97.

Makundi yaliyoshughulikiwa kati ya Desemba 2005 - Desemba 2008 ni kama ifuatavyo:-

Watoto

  1. Watoto 15,452 wanaoishi katika mazingira magumu wametambuliwa na wanapatiwa misaada ya kujikimu ikiwemo mahitaji ya shule ( sare na vifaaa) mavazi na matibabu.
  2. Kamati 240 zimeundwa ngazi ya mtaa / kijiji ili kushughulikia matatizo ya watoto walio katika mazingira hatarishi. Pia mafunzo yametolewa kwa kamati zote 240 juu ya wajibu wa kamati na malezi ya watoto.
  3. Jumla ya watoto 3,243 wamefaidika na mpango wa ajira mbaya kwa watoto na kujiunga na mafunzo ya ufundi, kuwalejesha shuleni na kuhakikisha wanapata haki zao ikiwa ni pamoja na huduma za afya, chakula na malazi.

Wazee

  1. Vikundi 7 vya wazee vinavyojishughulisha na shughuli za kiuchumi kama vile kilmo cha Mpunga, Mahindi, Ufugaji wa Nguruwe, Ngo'mbe, Mbuzi na Kuku wamepata mtaji wa tsh 59,789.51 kupitia mradi wa TASAF.
  2. Wazee watapata huduma ya matibabu bure katika hospitali ya mkoa, Wilaya na katika Zahanati na vituo vya afya vya umma.
  3. Kuingiza katika mipango ya bajeti shuguhli za kusaidia na kuboresha maisha ya wazee kama ilivyoainisha katika sera ya Taifa ya waazee, MKUKUTA na mwongozo wa TASAF.

Walemavu

Mkoa una jumla ya watoto walemavu 718 waliotambuliwa. Hadi kufikia juni 2008 watoto 279 (38%) waliotambuliwa wamepelekwa shuleni. Hii ni zaidi ya lengo la MKUKUTA la kufikisha 20% ifikapo mwaka 2010. Aidha Mkoa katika Halmashuri ya Wilaya ya Njombe ina mkakati wakuanzisha shule ya wenye ulemavu wa akili katika kata ya Makambako.

 

opyright © 2009 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, P.O.BOX 858, Iringa, TEL: 026 - 2702715, FAX: 026-2702082 / 2701888

[Go Home]