|
|
Afya
Mkoa wa Iringa hadi kufikia mwaka 2008 una jumla ya hospital 16 kati ya hizo 5 ni Serikali, 7 ni za Mashirika ya Dini, 4 za watu Binafsi. Mwaka 2005 kulikuwa na hospitali 14. Pia kuna vituo vya Afya 40, kati ya hivyo 23 ni vya Serikali, 15 ni vya Mashirika ya dini na 2 vya binafsi. Mwaka 2008 kulikuwa na vituo 36. Aidha Mkoa una jumla ya Zahanati 326 ambazo 231 kati ya hizo ni za Serikali, 70 za Mashirika ya dini, 25 za binafsi. Mwaka 2005 Zahanati zilikuwa 284. Idadi hii ya vituo vya ngazi mbalimbali inaufanya mkoa kuwa na jumla ya vituo vya huduma za Afya 382 wakati mawka 2005 kulikuwa na jumla ya vituo 336 sawa na ongezeko la vituo 46 (asilimia 13).
Lengo la Mkoa katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Huduma ya Afya ya Msingi (MMAM, 2010 - 2015) nikuhakikisha kuwa kila kijiji kuwa na Zahanati, kila kata kuwa na kituo cha Afya na kila Wilaya kuwa na Hospitali.
Mafanikio yaliyopatikana kuanzia mwaka 2005 hadi 2008 ni;
- Nyumba za watumishi wa Afya zimeongezeka kutoka nyumba 361 mwaka 2005 kufikia nyumba 377 mwaka 2008, sawa na ongezeko la nyumba 16 (sawa na 5%).
- Katika kipindi cha 2005 hadi 2008 ukarabati umefanyika katika vituo vya afya na Zahanati 72.
- Hospitali ya Mkoa nayo ilifanyiwa ukarabati mkubwa.
- Halmashauli za Wilaya ya Iringa na Kilolo zimepa Hospitali Teule 2 za Wilaya.
- Mahudhulio ya kina mama wajawazito yameongezeka kwa asilimia 11 kutoka wastani wa asilimia 44 hadi asilimia 55. Kiwango cha mama wajawazito wanaojifungua katika vituo vya tiba imeongezeka kutoka asilimia 54 mwaka 2005hadi kufikia asilimia 68 mwaka 2008.
- Vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka 147 kufikia 108 kwa kila akinamama 100,000 kuanzia mwaka 2005 hadi 2007.
- Bodi ya kamati za Afya za Hospitali na vituo vya afya zimeundwaatika Halmashauli zote isipokuwa Halmashauli mpya za Kilolona Njombe ili kusimamia utoaji wa huduma za Afya.
- Kiwango cha chanjo kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kimeongezeka kutoka asilimia 76 mwaka 2005kufikia asilimia 87 mwaka 2008.
- Vituo vya utoaji wa dawa za kupunguza makali kwa wagonjwa wa UKIMWI vimeongezeka kutoka vituo 3 mwaka 2005 kufikia vituo 42 mwaka 2008.
|